1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Barack Obama atarajiwa kuhutubia mkutano wa DNC

20 Agosti 2024

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, anatarajiwa kuhutubia kwenye mkutano wa chama cha Democrats unaoingia siku ya pili mjini Chicago.

https://p.dw.com/p/4jgxA
Barack Obama | Rais wa zamani wa Marekani
Rais mstaafu Barack Obama ambaye ni mmoja kati ya viongozi wenye ushawishi ndani ya chama cha Democratic anatarajiwa pia kuhutubia mkutano wa chama cha Democratic unaofanyika mjini Chicago Marekani, Agosti 20, 2024.Picha: Olivier Douliery/abaca/picture alliance

Hapo jana Rais Joe Biden aliagwa japo si rasmi. Biden, katika miaka iliyopita alikuwa makamu wa rais Barack Obama kwa muda wa miaka minane.

Baada ya Rais Biden kuhutubia na kuondoka Chicago, wajumbe sasa watatumia wiki nzima kuangazia mustakabali  wa wagombea wao, Kamala Harris na mwenzake gavana wa Minnesota,Tim Walz. 

Mkutano huo unatarajiwa siku ya Alhamisi kumteua rasmi Harris kuwa mgombea wa urais baada ya Rais Joe Biden mwezi uliopita kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais.