1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yamwita balozi wa Ujerumani mjini Tehran

Josephat Charo
24 Julai 2024

Iran imesema imemuita balozi wa Ujerumani mjini Tehran atoe maelezo baada ya kufungwa kituo kimoja cha kiislamu mjini Hamburg kwa madai kwamba kinalisaidia kundi la Hezbollah.

https://p.dw.com/p/4igjJ
Ubalozi wa Ujerumani mjini Tehran
Ubalozi wa Ujerumani mjini TehranPicha: Fatemeh Bahrami/AA/picture alliance

Iran imesema imemuita balozi wa Ujerumani mjini Tehran atoe maelezo baada ya kufungwa kituo kimoja cha kiislamu mjini Hamburg kwa madai kwamba kinalisaidia kundi la Hezbollah la nchini Lebanon na kwa kuwa na mafungamano na Iran.

Soma: Ujerumani yalipiga marufuku vuguvugu la Hezbollah

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema katika taarifa yake iliyochapishwa katika mtandao wa kijamii wa X kwamba kufuatia hatua ya polisi ya Ujerumani iliyovifunga vituo kadhaa vya kiislamu, balozi wa Ujerumani anatakiwa aende kwa wizara hiyo akatoe maelezo.