1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wakurdi wanakataa Iraq kutangazwa kuwa taifa la Kiislamu.

6 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnP

Wakurd wa Iraq wamekataa mapendekezo ya kutaka nchi hiyo itangazwe kuwa taifa la Kiislamu , wakati bunge la jimbo hilo la kaskazini lenye madaraka yake ya ndani , likijadili muswada wa katiba ya nchi hiyo kabla ya mkutano wa kitaifa utakaojadili katiba hiyo hapo kesho.

Massud Barzani , rais wa jimbo hilo la Wakurdi , amesema Wakurdi hawatarudi nyuma katika madai yao ambayo yanajumuisha suala la serikali ya majimbo ya Iraq, pamoja na kuunganishwa na eneo lenye mafuta la kaskazini la Kirkuk katika jimbo lao lenye madaraka ya ndani.

Wakati huo huo majeshi ya Marekani na yale ya Iraq yameshambulia eneo la waasi upande wa magharibi, eneo ambalo limekuwa la maafa kwa wanajeshi wengi wa Marekani , ikiwa wanajeshi 40 wa Marekani wameuwawa katika eneo hilo katika muda wa wiki mbili zilizopita.