1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Bomu lauwa watu 31 wanawake na watoto.

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9W

Nchini Iraq bomu lililolipuka katika wilaya inayokaliwa na Washia katika eneo la Sadr City limesababisha watu 31 kuuwawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wakati wakijipanga kuchukua mafuata ya kupikia.

Watu wengine 34 wameungua vibaya. Kundi ambalo halifahamiki sana la wapiganaji wa Kisunni limedai kuhusika na shambulio hilo.

Mjini Tikrit vichwa vya watu tisa, ikiwa ni pamoja na vya polisi kadha , vimekuwa vikitupwa kutoka katika gari iendayo mbio.

Ghasia hizo zinaingiliana na mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan , ambao umeanza kwa Wasunni wengi wa Iraq jana Jumamosi. Jeshi la Iraq limesema kuwa limemkamata Muntasir al-Jibouri, kiongozi wa kundi la wapiganaji la Ansar al-Sunna , kundi la wapiganaji lenye mahusiano na Al Qaida.

Kundi hilo katika ujumbe wake uliotolewa katika mtandao wa internet limekana kukamatwa huko. Jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi wake watatu wameuwawa kaskazini mwa Iraq.