ATHENS : Ugiriki yaripoti homa ya mafua ya ndege
18 Oktoba 2005Matangazo
Ugiriki imekuwa nchi nyengine kurepoti kesi ya homa ya mafua ya ndege wakati kirusi cha homa hiyo kikionekana kuenea barani kote Ulaya.
Wizara ya kilimo ya Ugiriki imesema kirusi hicho aina ya H5 kimegundulika kwenye mifugo ya kuku katika kisiwa cha Aegean cha Chios.Uchunguzi umekuwa ukifanyika kuthibitisha iwapo hicho ni kirusi thakili cha aina ya H5N1 ambacho tayari kimegunduliwa kwa ndege nchini Romania na Uturuki.
Hatua za tahadhari kuzuwiya kuenea kwa homa ya mafua ya ndege zimekuwa zikitekelezwa katika nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani.