1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assad: Juhudi za kurejesha uhusiano na Ankara hazijafanikiwa

26 Agosti 2024

Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema kuwa juhudi za kurekebisha uhusiano na Uturuki bado hazijafanikiwa hadi sasa.

https://p.dw.com/p/4ju0A
Aleppo türkische Ministerpräsident Recep Tayyip Erdogan und syrischer Präsident Baschar al-Assad
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisalimiana na mwenzake wa Syria Bashar Al-AssadPicha: Sana/epa/dpa/picture alliance

Katika hotuba aliyoitoa katika bunge la nchi hiyo, Al-Assad amesema juhudi za kurekebisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hazijakuwa na matokeo chanya licha ya nia ya dhati ya wapatanishi, akiashiria juhudi za upatanisho za Urusi, Iran na Iraq.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa ili juhudi hizo zifanikiwe, kwanza lazima sababu zilizopelekea kuvunjika kwa uhusiano kati ya nchi yake na Uturuki zijulikane na kuondolewa.

Soma pia: Erdogan asema huenda akamualika Assad kwa mazungumzo nchini Uturuki

Uturuki ilivunja uhusiano na Syria mnamo mwaka 2011 baada ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria wakati Uturuki iliunga mkono waasi waliotaka kumwondoa madarakani Assad. Assad mwenye anawachukulia waasi hao kama magaidi.

Kiongozi huyo wa Syria ameweka wazi kwamba anataka wanajeshi wa Uturuki waondoke nchini mwake, ingawa hilo sio sharti la mazungumzo.