1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan huenda akamualika Assad kwa mazungumzo Uturuki

7 Julai 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema anaweza kumualika mwenzake wa Syria Rais Bashar al Assad "wakati wowote kuanzia sasa" kama ishara ya maridhiano baada ya vita vya Syria vya mwaka 2011 kuyaharibu mahusiano yao

https://p.dw.com/p/4hz9m
Bashar Assad na Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Syria Bashar Al Assad na mwemzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Picha: BULENT KILIC/AFP/Getty Images

Matamshi ya Erdogan yanakuja baada ya mvutano ulioshuhudiwa wiki iliyopita, wakati magenge ya watu yalipomiminika mitaani yakiharibu biashara na mali za raia wa Syria mjini Ankara.

Uturuki ilikuwa na nia ya kuuangusha utawala wa Rais Bashar al Assad wakati vita vya Syria vilipoanza mwaka 2011 kwa kuwaunga mkono waasi waliotaka Bashar aondoke uongozini.

Erdogan hajaondoka uwezakano wa kurudisha uhusiano na Syria

Lakini hivi maajuzi Erdogan alisema huenda akayasawazisha mahusiano yake na Assad wakati serikali yake ikijaribu kuhakikisha  Wasyria wanaotaka kurudi nyumbani kwa hiari wanarejea salama.

Akizungumza na waandishi habari Erdogan amesema viongozi kama rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuwa mpatanishi katika mkutano wa viongozi hao wawili nchini Uturuki.