1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA:KESI YA MAUAJI YA HALAIKI YAANZA ARUSHA

28 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFx3
Kesi ya maafisa wa zamani watatu wa serikali ya Rwanda wanaoshtakiwa kwa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadaamu waliotenda hapo mwaka 1994 imeanza hapo jana mbele ya Mahkama ya kimataifa nchini Tanzania. Watuhumiwa hao watatu ambao wote wamekana mashtaka walikuwa ni watu wa karibu kwa Rais Juvenal Habyarimana ambaye kifo chake kutokana na kuanguka ndege hapo mwaka 1994 ndicho kilichochochea mauaji ya halaiki ambayo yamepelekea kuuwawa kwa takriban watu milioni moja.Wanaume hao watatu wanashtakiwa kwa kula njama ya kukitokomeza kizazi cha kabila la Watutsi walio wachache nchini Rwanda pamoja na Wahutu wenye misimamo ya wastani walio wengi nchini humo ambao walikuwa wakiupinga utawala wa Habyarimana. Mawakili wa utetezi wametaka Rais Paul Kagame aitwe mahkamani kutowa ushahidi kuhusiana na kuangushwa kwa ndege ya Habyarimana.