1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA, TANZANIA: Mahkama ya Kimataifa kuchunguza uhalifu kwa ajili ya

4 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvJ

Rwanda imewahukumu Wanyaruanda wawili waliokuwa waandishi wa habari, kifungo cha maisha kwa sababu ya kuchochea mauwaji mwaka 1994 nchini. Mahkama hiyo, ikiwapo Arusha, Tanzania, imekuja kutambua wakuu hao wana hatia kwa kuwa walitumia vituo vya Radio na Televizheni kuhimiza mauwaji dhidi Watutsi na Wahutu wenye siasa za wasitani wakati wa vita vya kiraia vya Rwanda. Mahkama imemhukumu pia mwengine watatu, kifungo cha miaka 35 gerezani kwa mashtaka kama hayo. Kiasi watu laki nane wanakisiwa kuwa waliuawa nchini Rwanda, baina ya Aprili na Julai, mwaka 1994.