1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA: Mahakama ya kimataifa yaanza kazi yake.

11 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOE

Mashtaka yanayowakabili maafisa wanne wa zamani wa jeshi la Rwanda akiwemo mkuu wa jeshi hilo Brigadier Generali Gratien Kabiligi yameanza tena katika mahakama ya kimataifa huko mjini Arusha nchini Tanzania.

Wakati huo huo makahama ya kimataifa ya umoja wa mataifa imeanza leo hii kikao chake cha wiki mbili kusikiliza malalamishi ya mwaka 1999 yaliyowasilishwa na jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya serikali ya Uganda kwa kuyavamia maeneo yake na kufanya mauaji ya kinyama kwa raia wa Kikongomani.

Serikali ya Kongo inataka mahakama hiyo itoe uamuzi wa kufanyika uchunguzi wa kuvuruga amani na unyang’anyi uliofanywa na wanajeshi wa Uganda.

Serikali ya Uganda imekanusha malalamiko hayo ya Kongo.

Kikao hicho kinaongozwa na jopo la majaji 15