1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyewashambulia watu Ujerumani ahukumiwa miaka 14 jela

23 Desemba 2022

Mahakama ya Ujerumani imemuhukumu kifungo cha miaka 14 gerezani, mwanaume mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuua na kudhuru mwili katika shambulizi la kutumia kisu kwenye treni mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4LMmA
Deutschland Messerangriff im ICE zwischen Regensburg und Nürnberg
Picha: Vifogra/AP Photo/picture alliance

Katika shambulizi hilo, watu wanne walijeruhiwa. Mwanaume huyo raia wa Palestina mwenye umri wa miaka 28 ambaye amekulia nchini Syria alitambuliwa kama Abdalrahman A. amekutwa na hatia katika mahakama ya Munich.

Shirika la habari la Ujerumani, DPA limeripoti kuwa waendesha mashtaka ambao walidai shambulizi hilo lilikuwa lenye msimamoi mkali wa kiislamu walitaka mahakama itoe hukumu ya kifungo cha maisha jela.

Aidha, mawakili wa mshtakiwa walisema mteja wao alikuwa mgonjwa na hangeweza kushtakiwa kwa uhalifu na walitaka aachiwe huru.

Shambulizi hilo lilifanyika katika treni za mwendo kasi, ICE iliyokuwa ikisafiri kutoka Passau kwenda Hamburg Novemba 6, mwaka 2021.