1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yatuma maombi kujiunga na kundi la BRICS

22 Julai 2023

Algeria imetuma maombi ya kujiunga na kundi la ushirikiano wa kiuchumi la mataifa matano la BRICS pamoja na kuwa mwanahisa wa benki ya maendeleo ya kundi hilo ikitoa ahadi ya kitita cha dola bilioni 1.5.

https://p.dw.com/p/4UFmz
Makao makuu ya BRICS
Makao makuu ya BRICSPicha: Fang Zhe/Xinhua/IMAGO

Taarifa hizo zimeripotiwa na kituo cha televisheni cha nchini Algeria cha Ennahar kikimnukuu rais Abdelmadjid Tebboune. Chombo hicho kimesema rais Tebboune alizungumzia suala hilo alipokuwa akihitimisha ziara yake nchini China mwishoni mwa wiki hii, ambapo alisema Algeria inataka kujiunga na kundi la BRICS kwa lengo la kufungua fursa mpya za kiuchumi.

Soma zaidi:BRICS yajadili uwezekano wa kujitanua na kujumuisha nchi zinazosafirisha mafuta 

Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika lina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi asili na limekuwa likijaribu kuimarisha sekta nyingine za kiuchumi kupitia ushirika na mataifa makubwa mfano wa China.

Kundi la BRICS linaloyajumuisha mataifa ya China, Brazil, India, Urusi na Afrika Kusini linazingatiwa kuwa mbadala wa makundi mengine ya ushirkiano ya kiuchumi yanayotawaliwa na mataifa ya magharibi.