1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa mambo ya nje wa BRICS wakutana Afrika Kusini

1 Juni 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazounda kundi la BRICS wanakutana leo nchini Afrika Kusini, wakati nchi hizo tano zikijipanga kukabiliana na ushawishi wa nchi za magharibi.

https://p.dw.com/p/4S399
BRICS | Gipfeltreffen 2017 in Xiamen
Picha: Wu Hong/AP Images/picture alliance

 Kikao chao ni maandalizi ya mkutano wa kilele unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mjini Johannesburg, ambao tayari unaandamwa na utata kutokana na uwezekano wa kuhudhuriwa na rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imemtolea waranti wa kukamatwa.

Nchi wanachama wa kundi hilo  ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini. Agenda ya mkutano wa leo haijawekwa bayana, lakini wachambuzi wanasema utalenga kuimarisha mshikamano miongoni mwa nchi washirika, na kufikiria kuwaingiza wanachama wapya.