1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alabama yamuua mtuhumiwa wa kwanza kwa nitrojeni

26 Januari 2024

Jimbo la Alabama limemuua kwa kutumia gesi ya nitrojeni mfungwa aliyepatikana na hatia ya mauaji, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Marekani kutumia mbinu hiyo ambayo mkuu wa haki za Umoja wa Mataifa ameielezea kama mateso.

https://p.dw.com/p/4bhbF
Kenneth Smith
Jela alikouawa Kenneth Smith kwa gesi ya nitrojeni.Picha: Micah Green/REUTERS

Kulingana na mwanasheria mkuu wa serikali, Kenneth Eugene Smith alitangazwa kuwa amekufa majira ya saa 2:25 usiku wa kuamkia leo.

Kenneth mwenye umri wa miaka 58 alikuwa akisubiri kunyongwa kwa zaidi ya miongo mitatu baada ya kukutwa na hatia ya mauaji mnamo mwaka 1988 kwa kumuua mke wa mhubiri, katika mauaji ya kulipwa.

Soma zaidi: Alabama kumuuwa mfungwa wa kwanza kwa niatrojini

Aliuawa katika gereza la Holman kwa kutumia gesi ya nitrogeni iliyowekwa ndani ya barakoa, na kumsababishia kukosa hewa.

Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema amesikitishwa pakubwa na tukio hilo, akiongeza kuwa mbinu hiyo iliyotumika inaweza kuelezewa kuwa ni ya mateso, kikatili, isiyo ya kiutu na ya kudhalilisha.
 
Alabama ni moja kati ya majimbo matatu ya Marekani ambayo yameidhinisha matumizi ya gesi ya nitrogen hypoxia kama njia ya mauaji, pamoja na Oklahoma na Mississippi.