1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alabama kumuuwa mfungwa wa kwanza kwa niatrojini

25 Januari 2024

Maafisa wa jimbo la Alabama nchini Marekani wanatazamiwa kumuuwa mfungwa kwa kutumia gesi ya naitrojini, mbinu ambayo haijawahi kutumiwa hapo kabla.

https://p.dw.com/p/4beWZ
Mlinzi wa jela
Mlinzi wa jelaPicha: AFP/Getty Images

Jimbo la Alabama linadai itakuwa ya kiutu lakini nao wakosoaji wanaiita kuwa ya kikatili na ya majaribio.

Kenneth Eugine Smith, mwenye umri wa miaka 58 aliyehukumiwa kwa mauaji, anatarajiwa ku katika gereza moja la kusini mwa Alabama leo usiku.

Mfungwa huyo alipaswa kuuliwa mwaka wa 2022 kwa kuchomwa shindano ya sumu lakini tukio hilo likasitishwa dakika ya mwisho kwa sababu maafisa walishindwa kumuwekea mpira wa kupitisha sumu.

Mawakili wa Smith walipambana mahakamani kusitisha utekelezaji wa adhabu hiyo ya kifo kwa kutumia naitrojini, wakihoji kuwa jimbo hilo linataka kumfanya Smith kuwa kesi ya majaribio ya mbinu hiyo mpya ya kuuwa ambayo inapaswa kuchunguzwa zaidi kisheria kabla ya kutumiwa kwa mfungwa.

Mahakama ya Juu ya Marekani jana iliikataa hoja ya Smith kuwa itakuwa kinyume cha sheria kufanya jaribio jingine la kumuuwa baada ya lile la kuchomwa shindano kushindwa.