1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu na majimbo

30 Mei 2024

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Afrika Kusini baada ya umma wa taifa hilo kushiriki uchaguzi wa taifa siku ya Jumatano, ambao unazingatiwa kuwa kipimo kwa chama cha ANC, kilicho madarakani kwa miaka 30.

https://p.dw.com/p/4gS0B
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea Afrika Kusini.
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea Afrika Kusini.Picha: Phill Magakoe/AFP/Getty Images

Hadi sasa asilimia 10 ya kura zimekwishahesabiwa na ANC imepata asilimia 42 ikifuatiwa na chama cha kileberali cha Democratic Alliance kilichojikingia asilimia 26 ya kura.

Soma pia:Raia wa Afrika Kusini washiriki uchaguzi Mkuu

Chama cha mrengo wa shoto cha mwanasiasa machachari Julius Malema kimo kwenye nafasi ya tatu kwa asilimia 8 kikifuatiwa na kile cha rais wa zamani Jacob Zuma cha uMkhonto weSizwe chenye asilimia 7. 

Katika uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2019 ANC ilishinda wingi wa viti bungeni baada ya kupata asilimia 57 kwenye matokeo ya mwisho. Matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa jana yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa juma.