1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika Kusini

Afrika Kusini: Moto wauwa zaidi ya watu 60 na kujeruhi

31 Agosti 2023

Watu wasiopungua 70 wamepoteza maisha na wengine 52 wamejeruhiwa kufuatia moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katikati ya mji wa Johannesberg nchini Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/4VnOa
Südafrika | Großbrand in Johannesburg
Picha: Shiraaz Mohamed/REUTERS

Kwa mujibu wa msemaji wa  idara ya huduma ya usimamizi wa masuala ya dharura, Robert Mulaudzi, moto huo umezuka usiku wa kuamkia leo Alhamisi.

Haikujulikana wazi kwa haraka kilichosababisha moto huo.

Kiasi watoto saba ni miongoni mwa waliouliwa kwenye mkasa huo wa moto ambao inaonesha huenda ndio moja ya mikasa mibaya zaidi ya moto iliyowahi kutokea hivi karibuni duniani. 

Soma pia:Watu 15 wafariki kwenye ajali ya moto kiwandani, Ufilipino

Wazima moto wamefanikiwa kuudhibiti moto huo kwa mujibu wa Mulaudzi.

Watu wameondolewa kwenye jengo hilo lililozunguushiwa uzio wa usalama huku shughuli  ya kutafuta wahanga ikiwa inaendelea.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW