1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa mataifa kufanya ziara nchini Pakisatan

Epiphania Buzizi13 Oktoba 2005

Mratibu wa shughuli za misaada ya dharura wa Umoja wa mataifa Jan Egeland amewasili nchini Pakistan leo hii kuthathimini madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi nchini humo.

https://p.dw.com/p/CHeb
Wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Pakistan
Wahanga wa tetemeko la ardhi nchini PakistanPicha: AP

Ziara hiyo inalenga kupanga mikakati ya kuwasaidia wahanga wa maafa hayo.

Ziara ya mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa anaifanya nchini Pakistan wakati idadi ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na tetemeko hilo ikiripotiwa kuongezeka hadi watu 23000.

Bwana Egeland ameahirisha ziara aliyokuwa amepanga kufanya nchini Indonesia ,ambako yalitokea maafa ya tsunami mwaka jana, ili aweze kuzungumzia suala la mwitikio wa kimataifa nchini Pakistan kufuatia maafa mabaya ya tetemeko lililotokea siku ya Jumamosi.

Maafisa wa Umoja wa mataifa nchini Pakistan wamesema kuwa Bwana Egeland atalitembelea eneo la maafa la Muzaffarabad huko Kashmir ambalo liko mikononi mwa Pakistan.

Mratibu wa misaada ya dharura wa umoja wa mataifa pia atakutana kwa mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Pakistan, maafisa wa Umoja wa mataiafa wanaofanya kazi nchini humo pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamehusika katika misaada ya dharura ya kimataifa.

Bwana Egeland amepongeza juhudi za mwitikio wa haraka wa Umoja wa Mataifa kufuatia maafa hayo ya tetemeko, ambapo maafisa wa Umoja huo walisafirishwa kwa ndege mara moja baada ya kupokea taarifa za janga hilo.

Hata hivyio siku tano baada ya kutokea tetemeko hilo,misaada ya kimataifa inayowasili katika eneo la maafa haitoshelezi mahitaji ya watu wapatao milioni mbili na nusu ambao wamebaki bila makaazi.

Waziri mkuu wa Pakistan Shaukat Aziz ambaye jana alizulu eneo la maafa la Muzaffarabad kwa mara ya kwanza tangu kutokea tetemeko hilo, amepongeza jumuiya ya kimataifa kwa misaada ambayo imetolewa kwa Pakistan, lakini akabainisha kuwa misaada zaidi inahitajika.

Waziri huyo mkuu wa Pakistan amesema kuwa misaada inayotolewa hivi sasa ni ya dharura, na bado Pakistan itahitaji misaada zaidi wakati wa awamu ya ukarabati mpya, akiongeza kwamba watu hawana budi kufikiria juu ya kipindi cha majira ya baridi ambacho kinakaribia.

Wachunguzi huru ambao wamewasili katika eneo lililokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi, wamesema kuwa hakuna utaratibu mzuri unaofuatwa katika kutoa misaada kwa walengwa, ambapo wahanga wa tetemeko hilo wanalazimika kugombania misaada hiyo.

Wakati huo huo ofisi ya Umoja wa mataifa inayoratibu masuala ya huduma za kiutu imeweka makao ya muda katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad na pia katika mji ulio Kaskazini wa Muzaffarabad.

Lakini juhudi za kutoa misaada zimzekabiliwa na vikwazo kutokana na milima mirefu pamoja na barabara zilizoharibiwa na vifusi vya maporomoko ya milima na hivyo kufunga njia ya kuelekea eneo la maafa.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa timu za waakozi kutoka mataifa mbali mbali hususan Uingereza,China,Ufaransa,Ujerumani,Ugiriki,JapanUturuki,Uholanzi,Poland,Urusi,Singapore na Korea ya Kusini wamepelekwa nchini Pakistan kusaidia katika juhudi za uokozi.

Lakini matumaini ya kuwapata watu walionusurika chini ya vifusi vya nyumba yanazidi kuyoyoma. Kwa sasa mtihani mkubwa wa kubainisha mwitikio wa kimataifa hauna budi kuthibitishwa na hatua zitakazofuata za kutoa misaada wakati wa kipindi ukarabati kitakachaofanyika majira mabaya ya baridi kali.

Mpaka sasa kuna dadili za kuanza kuzorota juhudi za kutoa misaada baada ya maafa ya mwaka jana ya Tunami nchini Indonesia, na pia maafa ya hivi karibuni ya kimbunga Katrina huko New Orleans nchini Marekani.

Waziri mkuu wa Pakistan amesema kuwa serikali imepata ahadi za misaada kimataifa kiasi cha dola za kimarekani milioni 350,wakati ambapo pia misaada iliyotolewa na wananchi wa Pakistan wenyewe inafikia dola zaidi ya milioni 16 na nusu.

Wakati huo huo rasi wa Pakistan Pervez Musharraf ambaye amaelihutubia taifa jana usiku kupitia televisheni, amebainisha kuwa Pakistan bado inahitaji misaada,na ameitoklea mwito jumuiya ya kimataifa kutoa misaada yoyote inayowezekana.

Wakati huo huo jeshi la Pakistan limekanusha ripoti iliyotolewa na nchi hasimu ya India kwamba wanajeshi wake wamevuka eneo la mzozo la mpakani la Kasmir ili kusaidia katika ukarabati baada ya uharibifu uliosababishawa na tetemeko la ardhi nchini Pakistan.

Vyombo vya habari vya kimataifa vilikuwa vimeiona hatua hiyo kama ishara ya umoja wa pande hasimu wakati wa maafa..

Msemaji wa jeshi la Pakistan Meja jenerali Shaukat Sultan, amewaambia waandishi habari kwamba madai hayo ni uongo usio na msingi wowote.

Pakistan na India zimekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo la mpaka la Kasmir, kila upande ukidai kuwa eneo hilo ni lake, suala ambalo lilizusha vita katika eneo hilo.