1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan: Makundi ya kihasimu ya yawafikiane kupokonywa silaha:

16 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0P

KABUL:
Nchini Afghanistan, makundi mawili ya kihasimu
ya makabila ya Kitajiki na Kiuzbeki yamekubalia
mapatano ya kupokonywa silaha baada ya mapigano
ya miezi kadha. Chini ya waangalizi wa UM,
serikali ya Kabul na mabingwa wa ukarabati wa
Kiingereza, wanamgambo wa makundi hayo mawili
Jamiat na Junbish, kuanzia Ijumaa ijayo
watazikabidhi silaha zao nzito, aliarifu
msemaji wa UM mjini Kabul. Mapatano hayo ya
kupokonywa silaha yatatumika katika mikoa yote
mitano ambamo wanamgambo hao wakiendesha
harakati zao za kupigana. Kwa kulingana na
tahtmini za UM, mapigano hayo yaliyodumu muda
mrefu kati ya wafuasi wa Jenerali wa Kiuzbeki
Rashid Dostum na Jenerali wa Kitajiki Atta
Mohammed yalipamba moto zaidi katika eneo la
Masaris Sharif, yakiwa ni mapigano makali
kabisa kuwa kutokea Afghanistan tangu
uangushwe utawala wa Taliban hiyo miaka miwili
iliyopita. Watu wengi waliuawa katika mapigano
hayo.