1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoIvory Coast

Ivory Coast yafungua dimba kwa ushindi wa mabao mawili

14 Januari 2024

Katika mashindano ya kandanda ya kugombea ubingwa wa mataifa ya Afrika (AFCON) mwenyeji Ivory Coast imelinda heshima.

https://p.dw.com/p/4bDeF
Mashabiki wa timu ya taifa ya Ivory Coast mjini Abidjan
Mashabiki wa timu ya taifa ya Ivory Coast mjini AbidjanPicha: CSM/Newscom World/IMAGO

Mchezaji wa kiungo, Seko Fofana alihitaji dakika nne tu kuliona lango la Guinea Bissau katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo mjini Abidjan.

Ivory Coast walijihakikishia ushindi baada ya Jean-Phillippe kufunga goli la pili katika nusu ya pili ya mchezo wa kundi A. Wanasoka wa Ivory Coast ambao wamewahi kuwa mabingwa wa Afrika mara mbili waliweza kuudhibiti mchezo kwa utulivu na kutengeneza nafasi za magoli.

Baadae leo Nigeria itakutana na Guinea ya Ikweta katika mechi nyingine ya Kundi A, na katika kundi B, Misri itaingia uwanjani na Msumbiji, wakati Ghana itamenyana na Cape Verde.