1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la ADF ladaiwa kuuwa watu 17 DRC

30 Mei 2023

Kundi la waasi wa ADF linadaiwa kuwauwa takribani watu 17 huko katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/4Rycq
Kongo I Soldaten während einer gemeinsamen Militäroperation gegen bewaffnete Kräfte in Beni
Picha: Alain Uaykani/Xinhua News Agency/picture alliance

Naibu Gavana  Sabiti Njiamoja amesema kundi hilo linalofungamanishwa na Dola la Kiislamu limefanya tukio hilo katika eneo la Bambuba- kisiki lililo katika mamlaka ya Beni.

Amesema Jumapili wamefanikiwa kuzikia miili 10. Mauwaji hayo yamefanyika Ijumaa na Alhamisi iliyopita. Mzozo umekuwa ukipamba moto kwa miongo kadhaa mashariki mwa Kongo, ambapo zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanapambana.

Soma pia: Watu 20 wameuawa katika mashambulio ya waasi wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mengi miongoni mwa makundi hayo yanagombania ardhi na kudhibiti maeneo ya  migodi ya madini, huku baadhi ya makundi yakiwa katika juhudi za ulinzi wa jamii zao.