1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 20 wauawa katika mashambulio mashariki ya Kongo.

9 Aprili 2023

Takriban watu 20 wameuawa katika mashambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lawama zinaelekezwa kwa waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi linalojiita Diola la Kiislamu IS.

https://p.dw.com/p/4PrAw
Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Takriban watu 20 wameuawa katika mashambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lawama zinaelekezwa kwa waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi linalojiita Diola la Kiislamu IS. Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo, Patrick Mukohe amefahamisha kuwa waasi hao wa ADF waliwavamia wakulima mwendo wa saa kumi jioni karibu na kijiji cha Enebula. Mukohe amesema watu hao wanaume na wanawake waliuawa katika eneo lililo umbali wa kilomita 30 magharibi mwa mji wa Oicha, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mwezi uliopita Marekani ilitoa zawadi ya hadi dola milioni 5 kwa taarifa kuhusu kiongozi wa kundi la ADF, Seka Musa Baluku.