1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgamb kutoka katika kundi la uasi la ADF wauwa 17 DRC

12 Machi 2023

Wanamgambo wanaoshukiwa kutoka katika kundi la uasi la ADF leo hii wanadaiwa kuwauwa takriban watu 17 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4OZTR
Kongo | Demokratische Republik Kongo DRC Soldaten
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Wanamgambo wanaoshukiwa kutoka katika kundi la uasi la ADF leo hii wanadaiwa kuwauwa takriban watu 17 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi wa kijiji cha Kirindera kilichopo jimbo la Kivu ya Kaskazini, Katembo Kahongya, amesema pamoja na idadi hiyo ya vifo kuna watu wengine wanne wamejeruhiwa. Amesema walitumia visu na silaha za moto kufanya mauwaji hayo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, gavana wa zamani wa Kivu Kaskazini, Carly Nzanzu, ameandika idadi ya walikufa imefikia 19, baada ya kundi la wanaohisiwa kuwa ADF kufanya mashambulizi katika kijiji.

Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya kundi hilo lenye mafungamano na wenye itikadi kali kufanya mauaji mengine ya watu zaidi ya 40 katika eneo hilo lenye machafuko.