1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Mahkama ya Haki za Binaadamu kuanza kazi Afrika

9 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkj
Mahkama ya Haki za Binaadamu ya Afrika inatazamiwa kuanza kazi hapo Januari 25 baada ya hati za kuanzishwa kwake kuridhiwa na mataifa wanachama 15 wa Umoja wa Afrika kama inavyohitajika.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema leo hii mahakama hiyo itasaidia mamlaka ya Tume ya Afrika ya Kulinda Haki za Binaadamu na Watu pamoja na haja ya kujenga bara lenye haki, lilioungana na la amani ambalo halitokuwa na hofu vita na ujinga.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mahkama hiyo pia itaimarisha kujizatiti kwa Umoja wa Afrika katika kufanikisha kuheshimiwa kwa haki za binaadamu na kanuni za msingi za kuvumiliana, mshikamano,usawa wa kijinsia pamoja na kuwepo kwa vitendo vya kibinadaamu barani humo.