1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zurich. Wafanyakazi ruksa kuingia Uswisi.

26 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEXa

Wapiga kura wa Uswisi wamepiga kura kufungua soko lao la kazi kwa wafanyakazi kutoka katika mataifa 10 mapya wanachama wa umoja wa Ulaya.

Kiasi cha wapigakura asilimia 56 wamesema ndio katika kura ya maoni iliyofanyika katika taifa hilo kuhusiana na pendekezo ambalo linawaruhusu wafanyakazi kutoka mataifa mapya wanachama wa umoja wa Ulaya kusafiri na kufanyakazi bila vikwazo nchini Uswisi.

Taifa hilo tajiri lililoko katika milima ya Alpine binafsi si mwanachama wa umoja wa Ulaya.