1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Zuma azindua ilani ya uchaguzi kwa kutoa ahadi lukuki

19 Mei 2024

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameahidi kubuni nafasi mpya za kazi na kupambana na uhalifu wakati akizindua ilani ya uchaguzi ya chama chake kipya kuelekea uchaguzi mkuu wa taifa hilo unaosubiriwa kwa shauku.

https://p.dw.com/p/4g34K
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob ZumaPicha: AP/picture alliance

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi waliokusanyika kwenye uwanja wa michezo wa Orlando mjini Johannesburg, Zuma amesema chama chake cha uMkhonto weSizwe kitajenga viwanda vipya ambavyo vitaajiri watu wengi na pia kitatoa elimu bila malipo kwa watoto wa nchi hiyo.

Vilevile ameahidi kuifanyika mabadiliko katiba ya Afrika Kusini ili kurejesha nguvu kubwa kwa watawala wa jadi akisema nafasi yao kwenye jamii imepunguzwa kwa majukumu mengi kuwekwa mikononi mwa mahakimu na majaji.

Chama hicho cha Zuma kimeimarika haraka na kinatazamiwa kutoa changamoto kubwa dhidi ya chama tawala cha African National Congress, ANC, wakati wa uchaguzi wa Mei 29.