1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Uchaguzi mkuu Misri waingia siku ya pili

11 Desemba 2023

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa nchini Misri katika siku ya pili ya zoezi hilo lililoanza Jana Jumapili na ambalo linatarajiwa kumalizika kesho Jumanne.

https://p.dw.com/p/4a0UJ
Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri akipiga kura mjini Cairo.
Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri akipiga kura mjini Cairo. Kiongozi huyo anawania muhula wa tatu madarakani.Picha: Egyptian Presidency Media Office via AP/picture alliance

Rais wa sasa Abdel Fattah el-Sisi ambaye anapambana kwenye kinya'ang'anyiro hicho na wagombea wengine watatu wa upinzani wasiokuwa na umaarufu, anatarajiwa kwa uhakika kushinda muhula mwingine.

Uchaguzi huo pia unafanyika katika wakati nchi hiyo yenye wakaazi milioni 102 ikikabiliwa na mgogoro wa kiuchumi ambapo  takwimu zinaonesha takriban thuluthi moja ya wananchi wanaishi katika umasikini.

Zaidi ya watu milioni 67 wana haki ya kupiga kura katika uchaguzi huo. Wagombea wengine wanaowania urais ni Farid Zahran anayeongoza chama cha upinzani cha Social Democratic, Abdel-Sanad Yamama akiongoza chama kikongwe cha kiliberali cha Wafd na Hazem Omar wa chama cha Republican.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.