1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Zimbabwe yashutumiwa kukiuka taratibu kabla ya uchaguzi

8 Agosti 2023

Zimbabwe inatarajia kuingia katika uchaguzi mkuu, huku tuhuma za uwezekano wa kuwepo ukiukaji taratibu za uchaguzi zikizizonga taifa hilo linalotawaliwa na chama kimoja tangu walipopata uhuru wao mwaka 1980.

https://p.dw.com/p/4UvIi
Simbabwe | Präsident Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe Emmerson MnangagwaPicha: Jekesai Njikizana/AFP/Getty Images

Wanaharakati kutoka kikundi cha Pachedu na mashirika ya kiraia wanasema, wamegundua dosari nyingi kuelekea uchaguzi huo, ikiwemo urejeleshaji wa vitambulisho vya kupigia kura. 

Tafadzwa Sambiri, ambae ni kiongozi mkuu wa kikundi hicho alipoongea na Shirika la Habari la Ufaransa AFP amesema, Vitambulisho nchini Zimbabwe vinakuja na nambari ya utambulisho ambayo inafaa iwe ya kudumu lakini havionekani kuwa hivyo kwa baadhi ya watu.

Lakini pia amesema walipata maelfu ya nambari za vitambulisho ambazo zilitumiwa na watu katika uchaguzi mkuu wa 2013 lakini namba hizo pia zimesajiliwa upya kwa jina tofauti kwa mwaka 2023.

Soma zaidi:Upinzani Zimbabwe waenda mahakamani baada ya zuio la mkutano 

Kundi hilo limesema limegundua mambo mengine yasiyo ya kawaida, ikiwemo watu waliokufa kusajiliwa upya au wengine kuandikishwa mara mbili, akitolea mfano wapiga kura 183 wameonekana kuishi katika nyumba moja kwenye viunga vya Harare.

Zimbabwe siasa I Nelson Chamisa
Maelfu ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CCCPicha: Zinyange Auntony/AFP/ Getty Images

Katika hatua nyingine, raia mmoja aliyezungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la AFP kwa jina bandia la Tendai, kwa kuhofia usalama wake amesema, Yeye na mkewe wataondoka nyumbani na kuelekea maeneo tofauti ili kupiga kura hali amabyo amesema sio ya kawaida. Sheria tata ya "uzalendo" yaanza kutumika Zimbabwe

Wawili hao wanaoishi pamoja katika mji wa Kadoma wamepangiwa vituo tofauti vya kupigia kura, na hilo ni mojawapo ya jambo ambalo wanaharakati wanaeleza ni makosa yanayozua hofu ya kuibiwa kura.
  
Suala hilo lilianza kujulikana kwa mara ya kwanza mwezi Mei, wakati mamlaka ya uchaguzi ilipotaka orodha hiyo ifanyiwe ukaguzi, na wengi wakaona dosari za majina yao kuondolewa na kukosewa.

shutuma dhidi ya Mnangagwa: Rais wa Zimbabwe akosolewa na Upinzani

Mongoni mwa waliokumbwa na kadhia hiyo ni  David Coltart, Waziri wa zamani wa elimu na mwanachama wa Chama cha Wananchi (CCC) ambae, baada ya kutafuta jina lake kutwa nzima ndipo alibaini kuwa amehamishwa kituo cha mbali zaidi na nyumbani kwake.

Davis ameeleza kuwa, Katika baadhi ya matukio wapiga kura kutoka ngome za chama tawala wanaonekana kuhamishwa kwa wingi katika maeneo yanayoegemea upande wa upinzani, hali inayoweza kupelekea siku ya uchaguzi wengine kujikuta wameenda mahali pasipofaa. Jambo linaloweza kuleta shida kwa maeneo ya vijijini ambako watu wana shida ya mtandao na usafiri.

Soma zaidi:SADC yatakiwa kukemea ukandamizaji nchini Zimbabwe 

Hata hivyo David amesema, Hakuna shaka kwamba chama cha ZANU-PF na rais Mnangagwa wamejipanga kufanya kila linalowezekana kumzuia Chamisa na chama cha 'Triple C' kushinda. Lakini amesema CCC imesalia na imani kuwa ina uungwaji mkono wa kutosha kushinda vizuizi hivyo.
   
Wanaharaka mbalimbali pia wanaeleza huenda, kura hiyo kwa kiasi kikubwa inatarajiwa kuwa ya marudiano kati ya Rais Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha ZANU-PF, na kiongozi wa CCC Wakili na Mchungaji Nelson Chamisa. 

Zimbabwe|Upinzani
Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Nelson ChamisaPicha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP/picture alliance

Nayo ripoti ya Shirika la Human Rights Watch imesema upigaji kura ujao utafanyika chini ya "mchakato wa uchaguzi wenye dosari kubwa" ambao haukidhi viwango vya kimataifa vya uhuru na haki. Ambapo Imetaja miongoni mwa masuala mengi, ni pamoja na kupitishwa kwa sheria kandamizi ili kuzima upinzani na matumizi ya vitisho, na vurugu dhidi ya wapinzani.

Raisi azikosoa nchi za Magharibi kwa kuiwekea Iran vikwazo

Katika uchaguzi huo, waangalizi wa kimataifa wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika, wamealikwa kufuatilia upigaji kura. Rais Mnangagwa ameapa kuwa uchaguzi utakuwa wa uhuru na wa haki.