1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zidane ajiuzulu

27 Mei 2021

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amejiuzulu kwa mara nyingine kukifundisha kikosi hicho mara moja, siku tano baada ya Madrid kushindwa kuchukua ubingwa wa ligi ya La Liga.

https://p.dw.com/p/3u34S
Champions League - Juventus v Olympique Lyonnais | Tor Memphis Depay
Picha: Reuters/P. Powel

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amejiuzulu kwa mara nyingine kukifundisha kikosi hicho mara moja, siku tano baada ya Madrid kushindwa kuchukua ubingwa wa ligi ya La Liga na kuruhusu watani wao wa jiji Atletico Madrid kuondoka na kombe hilo.

Madrid imethibitisha uamuzi huo wa Zidane na kusema kwenye taarifa yake kuwa "sasa ni wakati wa kuheshimu uamuzi wake na kuonyesha kuthamini taaluma yake, kujitoa na mapenzi yake kwenye klabu katika kipindi chote."

Kocha huyo raia wa Ufaransa alikuwa na mkataba hadi Juni 2022, lakini alikuwa tayari ameripotiwa kwamba alikuwa akiwaambia wachezaji wa Real Madrid kwamba mapema Mei ataondoka klabuni hapo, wakati msimu wa 2020-21 utakapomalizika.

Katika nyakati mbili kama kocha wa Real Madrid, Zidane alishinda Ligi ya Mabingwa

mara tatu na ligi ya Uhispania mara mbili, lakini ilimaliza msimu huu bila ya kombe lolote, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11.

Taarifa hiyo imesema Zidane ni miongoni mwa wachezaji watakaoendelea kuthaminiwa sana wakati wote na kuongeza kuwa anajua kwamba ni miongoni mwa wachezaji walioko kwenye mioyo ya mashabiki wa klabu hiyo na Real Madrid itabakia kuwa nyumbani kwake wakati wowote.