1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine iko tayari kupigania maeneo yaliyotwaliwa na Urusi

3 Juni 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake iko tayari kuanzisha mashambulizi ya kudhibiti tena maeneo yake yaliyonyakuliwa na Urusi.

https://p.dw.com/p/4S9Y0
Wolodymyr Selenskyj
Picha: John Moore/Getty Images

Akizungumza na Jarida la Wall Street, Zelensky amesema  hajui makabiliano hayo yatachukua muda gani lakini kile anachoamini ni kwamba watashinda vita hivyo.

Kiev inamatumaini kwamba mashambulio ya kuyatwaa tena maeneo yake yatabadilisha kabisa mkondo wa vita vinavyoendelea tangu Urusi alipoivamia nchi hiyo miezi 15 iliyopita. 

Ukraine imedungua makombora zaidi ya 30 ya Urusi

Wiki iliyopita Zelensky alisema wanasubiri silaha zaidi kutoka kwa mataifa ya Magharibi na magari ya kivita kabla ya kuanzisha shambulio hilo. Urusi inaendelea kudhibiti maeneo kadhaa Mashariki, Kusini na Kusini Mashariki mwa Ukraine.