1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Zelensky: Usambazaji wa silaha Ukraine umepungua

17 Novemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema usambazaji wa makombora muhimu kwa nchi yake umepungua baada ya mapigano kuzuka kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas mwezi uliopita

https://p.dw.com/p/4YzLU
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumzia hali ya msaada wa kibinadamu kwa Ukraine mnamo Oktoba 22, 2023
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Zelensky amewaambia waandishi wa habari kwamba silaha zinazopelekwa nchini humo zimepungua hasa makombora ya milimita 155 ambayo hutumiwa sana katika eneo la vita Mashariki na Kusini mwa nchi hiyo.

Urusi na Ukraine zimejizatiti kudumisha na kulinda hifadhi yao ya makombora baada ya takriban miaka miwili ya mapigano makali kati ya mataifa hayo mawili.

Korea Kusini yadai Pyongyang imeipelekea Urusi silaha

Korea Kusini imedai kuwa mshirika wa Urusi, Korea Kaskazini, imetuma mizinga milioni moja ili kuimarisha vita vya Urusi nchini Ukraine kwa kubadilishana na ushauri kuhusu teknolojia ya satelaiti.

Wakati huo huo Ujerumani imesema wiki hii kwamba Umoja wa Ulaya hautafikia lengo la mwaka mmoja la kupeleka  makombora milioni moja nchini Ukraine, kwasababu Umoja huo unakabiliwa na changamoto katika kupata silaha hizo.