1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Nitamkabidhi Biden "mpango wa ushindi" mwezi huu

13 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo Ijumaa kwamba atakutana na mwenzake wa Marekani, Joe Biden, mwezi huu kuwasilisha kile alichokiita “mpango wa ushindi” wa namna ya kumaliza vita vya nchi yake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4kcAy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.Picha: Daniel Roland/AFP/Getty Images

Tangazo la Zelensky limejiri mnamo wakati Biden anatarajiwa kujadiliana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kuhusu ikiwa Ukraine inaweza kuruhusiwa kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya Urusi.

"Nitawasilisha mpango wa ushindi, ambalo ni mfumo wa masuluhisho yaliyofungamana, ambayo yataipa Ukraine nguvu ya kutosha kumaliza vita na kupata amani." Alisema Zelensky

Soma pia:Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni usiku kucha
Ukraine inazishinikiza Marekani na Uingereza kuondoa vikwazo vya kuyatumia makombora ya masafa marefu iliyopewa nchi hizo.