1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaonya NATO kujiingiza kwenye vita vyake na Ukraine

13 Septemba 2024

Rais Vladimir Putin amesema ikiwa mataifa ya Magharibi yatairuhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu kushambulia ndani ya Urusi, itamaanisha kwamba Jumuya ya Kujihami, NATO, inajiingiza kwenye vita hivyo.

https://p.dw.com/p/4kaoO
Nakili kiunganishi
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Sputnik/Gavriil Grigorov/Pool via REUTERS

Putin ameonya kwamba ataichukulia hatua kama hiyo kama mataifa ya NATO, ambayo ni pamoja na Marekani na mataifa ya Ulaya, yanapambana na Urusi, hali itakayobadilisha uhalisia wa vita hivyo.

Amesema hayo alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari mjini St Petersburg na kuongeza kuwa watalazimika kufanya maamuzi kwa kuzingatia kitisho watakachokuwa wanakabiliwa nacho, bila ya kutoa maelezo zaidi.

Biden, Starmer kujadili silaha za masafa marefu kwa Ukraine

Kiev mara kadhaa imeziomba Marekani na Uingereza kuruhusu majeshi yake kutumia makombora ya masafa marefu kushambulia ndani ya Urusi. 

Marekani imeiruhusu Kyiv kutumia silaha zake kushambulia ndani ya Urusi, ikiwa maeneo hayo yatakuwa karibu na mpaka wa mji wa Kharkiv, unaozingirwa na mapigano makali.