1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la UN

14 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4WJHC
UN Generalversammlung Video Volodymyr Zelensky
Picha: Angela Weiss/AFP

Hayo ni kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Zelensky mjini New York tangu Urusi ilipoivamia Ukraine miezi 18 iliyopita.

Guterres  amesema ingawa ni jambo gumu kuwezekana, anatarajia atapata fursa ya upatanishi ili kuwepo mazungumzo ya amani.

Hata hivyo Guterres amesisitiza kuwa hatarajii mafanikio yoyote ya kidiplomasia katika Mkutano huo unaowaleta pamoja zaidi ya wakuu 140 wa nchi na serikali, pamoja na maafisa kutoka mashirika ya kiraia na yasiyo ya kiserikali.