1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky na Biden kuhudhuria mazungumzo ya ulinzi wa Ukraine

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

MKutano huo utakaofanyika wiki ijayo kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein karibu na mji wa Francfurt hapa nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4lRrG
Marekani ni mshirika mkuu wa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi
Marekani ni mshirika mkuu wa Ukraine katika vita vyake dhidi ya UrusiPicha: UPI Photo/IMAGO

Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja viongozi zaidi ya  50 washirika wa Ukraine, akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden.

Zelensky amesema leo kwamba kwenye mkutano huo atawasilisha hatua za wazi na thabiti ili kukomesha vita. Huku akiongeza kuwa Urusi inaweza kusimamishwa na nia ya washirika wetu na kuimarishwa kwa Ukraine.

Kwenye mkutano wa Septemba, huko Ramstein, Zelensky aliomba silaha za ziada ili kurudisha nyuma vikosi vya Urusi vinavyosonga mbele. Mkutano huo utafanyika katika wakati muhimu kwa Ukraine kabla ya uchaguzi wa Marekani mwezi ujao.

Uchaguzi huo unaweza kutia kiwingu uungwaji mkono ambao serikali ya Kyiv inapata kutoka kwa mfadhili wake mkuu, Marekani.