SiasaUkraine
Zelensky: Lazima Ukraine iwe chonjo na Belarus
11 Januari 2023Matangazo
Zelensky ameyasema hayo leo baada ya kulitembelea eneo la Lviv ambako amezungumzia ulinzi wa mpaka, hali ya usalama kaskazini magharibi mwa Ukraine na hali ya operesheni katika mpaka na Jamhuri ya Belarus na hatua za kukabiliana na mashambulizi katika maeneo hayo.
Afisi ya Zelensky imesema rais huyo pia ameshiriki shughuli ya kuwakumbuka wanajeshi wa Ukraine waliouwawa katika mapigano kufuatia uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka uliopita.
Mapiganao makali yameripotiwa leo huko Soledar.