1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Zelensky kuuhutubia mkutano wa G7

6 Desemba 2023

Japan, mwenyekiti wa kundi la nchi tajiri kiviwanda G7 imesema rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atajiunga kwenye mkutano wao wa kilele kwa njia ya vidio, saa chache baada ya kukwepa mkutano na maseneta wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4Zpeu
Ukraine | vita | Rais Volodymir Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymir ZelenskyPicha: Presidential Office of Ukraine/SvenSimon/picture alliance

Mkutano huo utakaoanza baadae hii leo na kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, utatoa nafasi kwa Zelensky kujiunga na awamu ya kwanza ya mazungumzo na viongozi wa G7.

Kulingana na afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani, kando na masuala ya Ukraine mkutano huo pia utajadili mgogoro wa Mashariki ya Kati, msaada kwa mataifa yanayoendelea na masuala ya teknolojia ya akili ya kubuni. Juhudi za Ukraine pia kujiunga na Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa masuala magumu yatakayojadiliwa.

Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kufuatia msaada uliozuiliwa

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Oban aliye na mahusiano ya karibu zaidi na Putin ikilinganishwa na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya ametaka maamuzi muhimu juu ya Ukraine kuwekwa nje ya ajenda ya mkutano huo. Geert Wilders, Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Uholanzi, kinachotaka kusitisha msaada wa silaha kwa Ukraine pia ametilia shaka nchi yake kuendelea kuiunga mkono Ukraine.

Bunge la Marekani lagawika kuhusu msaada kwa Israel na Ukraine

Hata hivyo baada ya mkutano wa Novemba wa kundi la G7 kukamilika mjini Tokyo, kundi hilo lilisema uungaji mkono wake kwa kiev hautayumba na kwamba wameamua kusimama na ukraine kwa muda wote. Mataifa ya G7 ni pamoja na Marekani, Japan, Ujerumani, Ufaransa Uingereza Italia na Canada pamoja na Umoja wa Ulaya. Hadi mwaka 2014 Urusi ilikuwa miongoni mwa kundi hilo lililojulikana wakati huo kama G8.

Uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine unapungua

Japan G7
Mawaziri wa nchi za nje wa kundi la G7 katika mkutano wao a mwezi Novemba uliofanyika mjini Tokyo Picha: Tomohiro Ohsumi/AP Photo

Takriban miaka miwili tangu Urusi ianzishe uvamizi wake nchini Ukraine, dalili zinaendelea kuonekana kuwa uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine unapungua kama ilivyo kwa mashambulizi katika uwanja wa mapambano na pia wakati mapato ya mafuta ya rais wa Urusi Vladimir Putin yakiongezeka.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G7 wakutana nchini Japan

Awali rais huyo wa Ukraine Volodymir Zelensky aliufuta mkutano wake na maseneta wa Marekani uliotarajiwa kufanyika pia kupitia njia ya vidio, na Zelensky alinuia kuomba ufadhili zaidi kwa taifa lake linalokumbwa na vita. Alitaka kuwaomba kuunga mkono kura ya msaada wa dharura kwa kiev wa dola bilioni 60.

Urusi yarusha makombora, droni 23 kuelekea Ukraine

Huku hayo yakiarifiwa Zelensky pamoja na taarifa za jeshi nchini Ukraine zimesema ndege ya kivita ya Urusi aina ya Su 24 ilidunguliwa karibu na kisiwa cha bahari nyeusi cha Snake wakati msururu wa ndege zisizo na rubani zikiendelea kuvurumishwa katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.

Kamanda wa Jeshi la angani la Ukraine Mykola Oleshchuk amesema ndege ya Urusi ilidunguliwa wakati ilipojaribu kushambulia eneo la Odesssa.

Ujerumani: Hatutaiacha Ukraine kwenye vita peke yake

afp/dpa