1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky kuitembelea Poland siku ya Jumatano

3 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuitembelea Poland siku ya Jumatano katika ziara nyingine ya nadra nje ya nchi tangu uvamizi wa Urusi mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4PeKh
Ukraine Kiew | Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: Genya Savilov/AFP

Hayo yametangazwa leo na msemaji wa rais wa Poland Andrzej Duda kupitia ukurasa wa Twitter. Hii itakuwa ziara ya pili ya Zelensky nchini Poland baada kuitembelea nchi hiyo mnamo mwezi Disemba katika safari iliyompeleka pia Marekani.

Ratiba ya kiongozi huyo inajumuisha mkutano na raia wa Ukraine waliopewa hifadhi ya ukimbizi nchini Poland. Poland inazingatiwa kuwa mshirika muhimu wa serikali mjini Kyiv katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Ziara ya Zelensky inafanyika siku kadhaa baada ya Ukraine kutangaza mipango ya kununua magari 100 ya kivita kutoka Poland kupitia ufadhili utakaotolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya.