1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Hakuna ardhi ya Ukraine iliyopotea hadi sasa

Josephat Charo
20 Juni 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kufikia sasa hawajapoteza ardhi yoyote katika operesheni yao dhidi ya vikosi vya Urusi.

https://p.dw.com/p/4SoO2
Rais wa Ukraine Volodimyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodimyr ZelenskyPicha: DENIS BALIBOUSE/REUTERS

Akizungumza katika hotuba yake jana jioni Zelensky alisema baadhi ya wanajeshi wa Ukraine wanasonga mbele na katika baadhi ya maeneo wanazilinda sehemu zao na kuyakabili mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi na kuongeza mashambulizi.

Kwa mara nyingine tena rais Zelensky ameahidi kuwa bendera ya Ukraine hatimaye itapeperuka tena katika maeneo yote yanayokaliwa kusini na mashariki mwa Ukraine.

Urusi ilianzisha uvamizi kamili dhidi ya jirani yake Ukraine mnamo Februari 24 mwaka 2022 na imekuwa ikifanya vita vya kichokozi tangu wakati huo.