1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Maafisa wandamizi, magavana watimuliwa mabadilikoUkraine

25 Januari 2023

Ukaine imewafuta kazi magavana wa mikoa mitano iliyoko kwenye uwanja wa vita na maafisa kadhaa wengine wandamizi, katika mbadiliko makubwa zaidi ya uongozi wa wakati wa vita tangu uvamizi wa Urusi ulioanza mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4MeLG
Ukraine's President Zelenskiy attends a phone call with Britain's Prime Minister Sunak in Kyiv
Picha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Miongoni mwa zaidi ya maafisa 10 wanadamizi waliojiuzulu au kufukuzwa leo ni magavana wa mikoa ya Kyiv, Sumy, Dnipropetrovsk, Kherson na Zaporizhzhia.

Mikoa yote hiyo mitano imekuwa maeneo muhimu ya mapambano katika kipindi cha mwaka uliyopita, na kuwapa magavana wake umuhimu usio wa kawaida wa kitaifa.

Naibu waziri wa ulinzi, naibu mwendesha mashtaka, naibu mkuu wa ofisi ya rais Volodymyr Zelenskiy na manaibu waziri wawili wanaohusika na maendeleo ya mikoa ni miongoni wa wengine walioondoka kwenye nafasi zao.

Ukraine Kiew Generalstaatsanwaltschaft
Naibu mwendesha Mashtaka wa Ukraine ni miongoni mwa maafisa wandamizi walioachishwa kazi.Picha: STR/NurPhoto/picture alliance

Baadhi, japo siyo wote, walikuwa wamehusishwa na madai ya rushwa. Ukraine ina historia ya rushwa na utawala dhaifu, na inakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuonesha kuwa inaweza msimamizi wa kuaminika wa mabilioni ya dola za msaada wa mataifa ya magharibi.

Soma zaidi: Ukraine yaahidi mabadiliko ya maafisa wa serikali

Rais Zelenskiy aliahidi huko nyuma kushughulikia tatizo la rushwa iliyokithiri kaika ngazi zote za serikali, katikati mwa madai ya kuchukuwa hongo na votendo vya ukosefu wa maadili.

'Jibu kwa matakwa ya umma'

Msaidizi wa Zelenskiy Mykhailo Podolyak, katika ujumbe wa Twitter alisema "Rais anaona na anasikia. Na anashughulikia moja kwa moja matakwa muhimu ya umma -- ambayo ni haki kwa wote.

Safisha safisha hiyo imekuja siku mbili baada ya naibu waziri wa miundombinu kukamatwa na kushtumiwa kujipatia kiasi cha dola laki nne kutoka kwenye kandarasi za kununua majenerata, katika moja ya kashfa kubwa za kwanza za rushwa tangu kuanza kwa vita miezi 11 iliyopita.

Ukraine | PK Kyrylo Tymoshenko
Naibu mkuu wa ofisi ya rais Kyrylo Tymoshenko pia aliachia nafasi yake.Picha: Evgen Kotenko/Ukrinform/abaca/picture alliance

Hayo ni mabadiliko ya nadra katika uongozi wa wakati wa vita mjini Kyiv ambao umeonekana kuwa imara na tulivu.

Soma pia: Poland yaongeza shinikizo la kutuma vifaru Ukraine

Kando na kulisafisha shirika la kijasusi mnamo Julai, Zelenskiy ameendelea kubaki kwa sehemu kubwa na timu yake alioiunda kwa sehemu kubwa na wanagenzi wenzake wa kisiasa, ambao muigizaji huyo wa zamani wa televisheni aliingia nao madarakani alipochaguliwa kwa kishindo mwaka wa 2019.

Katika hatua nyingine tofauti, uamuzi uliyosubiriwa kwa muda mrefu juu ya iwapo washirika wanaweza kupeleka vifaru vizito vilivyotengenezwa Ujerumani nchini Ukraine, hatimaye umefika Berlin, baada ya Poland kusema imewasilisha rasmi ombi lake.

Chanzo: Mashirika