1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Dhamira ya kisiasa inahitajika kuisaidia Ukraine

4 Machi 2024

Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine amewarai washirika wake wa magharibi kuonesha dhamira ya kisiasa kwa kuipatia nchi yake mahitaji ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4d7rE
Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine
Rais Volodomyr Zelensky wa UkrainePicha: Adnan Beci/AFP/Getty Images

Amesema hilo litasaidia kuepusha kile amekitaja kuwa "miongoni mwa fedheha kubwa" kwa ulimwengu pale historia itakapoandikwa miaka inayokuja.

Akionekana kuwa mwenye ghadhabu, Zelensky ameitumia hotuba yake ya kila siku kwa taifa kuitaka dunia kumzuia rais Vladimir Putin wa Urusi kugeuza vita kuwa "mtaji" akimtuhumu kiongozi huyo kuwa anapendelea "vita na mauaji"

Zelesky ametoa mwito huo katika wakati mpango wa Marekani wa kitia cha dola bilioni 95 unaojumuisha kuipatia Ukraine msaada ziada wa kijeshi umekwama kutokana na mivutano ndani ya bunge mjini Washington.

Amesema nchi yake inasubiri mahitaji ambayo ni muhimu kwa ajili ya vikosi vyake kuendelea kupambana na amehimiza ulazima wa kuwepo dhamira ya kisiasa kuwezesha msaada kuafikiwa na kutumwa Ukraine.