1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky: Mashambulizi ya Urusi huko Kherson ni ya kigaidi

4 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi ya Urusi katika eneo la mashariki la Kherson na kuyaita "mashambulizi ya kigaidi."

https://p.dw.com/p/4ZjWd
Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Watu wawili wameuawa katika jumla ya mashambulizi 20 ambayo Zelensky amesema yamezilenga nyumba, barabara na hospitali eneo hilo.

Kulingana na utawala wa kijeshi wa Ukraine, mkoa wa Kherson ulioko katika mto Dnipro umekuwa ukilengwa kwa mashambulizi ya Urusi na kuanzia Jumamosi pekee, karibu mabomu 400 yamefyetuliwa eneo hilo. Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine kama Mariinka, Avdiivka na Bakhmut.

Ukraine imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Urusi  uliodumu kwa zaidi ya miezi 21, na mashambulizi yake ya kujihami yaliyozinduliwa katika majira ya joto mwaka huu, hadi sasa bado hayajakidhi matarajio yake.