1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asema upo uwezekano wa makubaliano juu ya Crimea

28 Agosti 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema kuna uwezekano wa kufikia makubaliano juu ya Rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na Urusi mwaka 2014 badala ya kutumia nguvu.

https://p.dw.com/p/4VdgR
Krim Plattform Ukraine Kyiv, Volodymyr Selensky
Picha: via REUTERS

Aliyasema hayo kwenye mahojiano ya siku Jumapili (Agosti 27) na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchini humo mapema Jumatatu. 

Zelensky alisema angelipendelea suluhu ya kisiasa kwa ajili ya Crimea kwa kuwa itahusisha wahanga wachache.

Soma zaidi: Putin ataka wapiganaji binafsi kula kiapo kwa taifa

Rais huyo wa Ukraine alisisitiza kwamba hakutaka kuvihamishia vita kwenye ardhi ya Urusi kwa kuwa lengo lao ni kuyakomboa maeneo ya Ukraine.

"Ikiwa tungelisonga mbele hadi kwenye maeneo ya Urusi, wangelihatarisha kukosa misaada kutoka Magharibi." Alisema Zelensky.