1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asema operesheni dhidi ya Urusi imeanza

11 Juni 2023

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesema kuwa operesheni ya kujibu mashambulizi ya vikosi vya Urusi yameanza. Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu operesheni za wanajeshi wake.

https://p.dw.com/p/4SRXc
Ukraine | Videoansprache von Wolodymyr Selenskyj
Picha: The Presidential Office of Ukraine

Urusi imeripoti kuyazuia mashambulizi ya Ukraine katika upande wa mashariki na Kusini katika siku za karibuni. Zelensky alisema anafanya mawasiliano ya kila siku na makamanda wake wa kijeshi, akiwemo mkuu wa majeshi Valery Zaluzhny, na kuwa kila mmoja ana matumaini na mashambulizi dhidi ya Urusi.

Soma pia:Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mji wa bandari wa Odessa nchini Ukraine

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alifanya ziara ya kushtukiza mjini Kyiv hapo jana. Trudeau, mwenye umri wa miaka 51, aliiahidi Ukraine msaada wa kijeshi wa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 375, akiongeza kuwa Canada itakuwa sehemu ya mpango wa kimataifa wa kuwapa mafunzo marubani wa Ukraine wa ndege za kivita.