1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky huenda akamfuta kazi mkuu wake wa majeshi

5 Februari 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema anatafakari uwezekano wa kumfuta kazi afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo, Jenerali Valerii Zaluzhnyi.

https://p.dw.com/p/4c2oq
Mkuu wa majeshi wa Ukraine Valerii Zaluzhnyi
Mkuu wa majeshi wa Ukrain Jenerali Valerii ZaluzhnyiPicha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema anatafakari uwezekano wa kumfuta kazi afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo,Jenerali Valerii Zaluzhnyi.

Rais Zelensky amekiambia kituo cha televisheni cha Italia RAI,katika mahojiano yaliyorushwa jana Jumapili,kwamba anafikiria kuchukuwa hatua hiyo kama sehemu ya mpango mpana wa kuelekea mwanzo mpya nchini Ukraine. Tangazo la kiongozi huyo limeishtuwa Ukraine na kusababisha wasiwasi kwa washirika wa nchi hiyo iliyoko vitani na Urusi.

Soma: Rais wa Ukraine awatembelea wanajeshi wake katika mstari wa mbele wa vita

Katika ufafanuzi alioutowa kupitia mahojiano hayo,rais Zelensky pia ameweka wazi kwamba hafikirii tu kufanya mabadiliko jeshini bali anataka pia kuwaondowa viongozi kadhaa waliono serikalini.

Kwa mujibu wa  ripoti za vyombo vya habari vya ndani ya Ukraine na nchi za Magharibi,wiki iliyopita rais huyo alimuomba mkuu wa majeshi   Zaluzhnyi ajiuzulu lakini jenerali huyo alikataa.Rais Zelensky amekuwa katika mvutano kwa muda na jenerali wake huyo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW