1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ameteua Umyerov waziri wa ulinzi wa Ukraine

4 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Vlodymry Zelensky amemteua Rusten Umyerov kuwa waziri mpya wa ulinzi.

https://p.dw.com/p/4VuKY
Ukraine Präsident Selentskji
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemteua Rustem Umyerov kuwa waziri mpya wa ulinzi kuchukua nafasi ya Oleksii Reznikov katika hatua ambayo imetarajiwa kwa muda. Umyerov ni mkuu wa Fuko la taifa la mali ya Ukraine.

Akizungumza katika hotuba yake jana jioni kwa njia ya video Zelensky alisema atawasilisha pendekezo bungeni kuridhia uamuzi wake.

Katika ujumbe wake Zelensky aidha alisema anaamini wizara inahitaji mitazamo mipyana mifumo mingine ya mawasiliano na jeshi na jamii kwa upana wake.

Uamuzi huo umetangazwa kufuatia ripoti katika vyombo vya habari vya Ukraine kwamba Reznikov angeondolewa katika nafasi yake. Reznikov pia alisema mara kwa mara kwamba alikuwa tayari kuondoka lakini ilibidi mrithi wake apatikane. Alisema alikuwa amezungumza na rais Zelensky kuhusu kushika wadhifa mwingine.

(dpa)