1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kulipiza kisasi baada ya kuuwawa watu 4 Ukraine

14 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kulipiza kisasi kufuatia shambulizi lililosababisha vifo vya watu wanne wa familia moja katika jimbo la Kherson, kusini mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4V7qL
Ukraine Kiew | Videoansprache Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

Zelensky amesema kupitia ukurasa wa Telegram jana Jumapili kwamba hakuna uhalifu wa Urusi ambao hautajibiwa.Mamlaka za Ukraine zimesema watu saba wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika jimbo la Kherson pekee na kuongeza kuwa familia hiyo ilishambuliwa asubuhi ya jana. Utawala wa kijeshi wa eneo hilo umetangaza siku ya leo kuwa ya maombolezo, wakati Urusi ikiendelea kushambulia mali, majiji na miji. Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 9,000 wameuawa hadi sasa.