1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky alaani mauaji ya mateka kukatwa vichwa

12 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo ameilaani Urusi kwa kitendo cha kuuliwa kwa kukatwa kichwa mateka wa kivita wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4PwhG
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine Picha: Omar Marques/Getty Images

Kitendo hicho kimeoneshwa kwenye video iliyosambazwa katika mitandao ya kijami. Zelensky amesema katika ujumbe wake kuwa, huo ni unyama mkubwa.

"Hakuna mtu duniani anayeweza kupuuza unyama kama huu. Jinsi wanavyouwa kiurahisi kabisa. Ni lazima dunia iione Video hii ya mauaji ya mateka wa kivita wa Ukraine. Videohii inaonesha hulka ya Urusi jinsi ilivyo. Hawa ni viumbe wa aina gan?.  si kitu kwao. Mwana, kaka, mume, mtoto wa mtu. Hii ni video ya Urusi ikijaribu kufanya haya kuwa hali mpya ya kawaida. Tabia ya kuharibu maisha."

Rais huyo ameapa kuleta haki kwa taifa lake lililokumbwa na vita.