1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky akerwa na viongozi kutohudhuria mkutano wa Uswisi

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya viongozi wa dunia kususia mkutano wa kilele wa amani kwa ajili ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4gXp7
Rais wa Volodymir Zelensky ahudhuria mkutano wa usalama Singapore
Rais wa Volodymir Zelensky ahudhuria mkutano wa usalama SingaporePicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/HANDOUT/AFP

Zelensky ameyasema hayo leo Jumapili katika kongamano la usalama nchini Singapore, ambako ameomba msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine.

"Tunasikitishwa kwamba baadhi ya viongozi wa dunia bado hawajathibitisha kushiriki katika mkutano huo wa amani. Kwa bahati mbaya, kuna majaribio ya kuvuruga mkutano huo. Hatutaki kuamini kwamba hii ni tamaa ya mamlaka ya ukiritimba duniani, kunyima jumuiya ya kimataifa fursa ya kuamua juu ya vita na amani na kuacha mamlaka hii mikononi mwa mmoja au wawili.", alisema Zelensky. 

Rais Zelensky amesema ziara yake huko Singapore ni katika umuhimu wa kupata ungwaji mkono wa nchi za Asia-Pacifiki kwa ajili ya mkutano ujao wa siku mbili wa amani ya Ukraine huko Uswisi katikati mwa mwezi huu.