1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Zelensky azungumza na Erdogan kuhusu amani ya Ukraine

21 Oktoba 2023

Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki hii leo yaliyotuama juu ya njia ya kupatikana tena amani nchini Ukraine, usalama wa chakula na hali kwenye kanda ya Mashariki ya Kati

https://p.dw.com/p/4Xr6a
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky akiwa Odessa mnamo Oktoba 13, 20203
Rais wa Ukraine Volodymr ZelenskyPicha: Presidential Office of Ukraine/SvenSimon/picture alliance

Zelensky amesema yeye na rais Erdogan wamejadili kuhusu duru mpya ya mazungumzo ya kusaka amani ya Ukraine inayotarajiwa kufanyika kwenye visiwa vya Malta pamoja na dhima ya Uturuki kwenye majadiliano hayo. Kadhalika wawili hao waligusia mzozo wa Mashariki ya Kati na kukubaliana umuhimu wa kulindwa raia na kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa.

Soma pia: Zelenskiy ataka marafiki wa Ukraine wasiisahau baada ya kuzuka vita vya Israel na Hamas

Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Urusi imeendeleza hujuma zake kusini na mashariki mwa Ukraine kwa kufyetua makombora yaliyosababisha vifo vya watu watatu na kujeruhiwa wengine wanne. Mashambulizi hayo yameulenga mkoa wa Kherson na ule wa nyumbani kwa rais Zelensky wa  Dnipropetrovsk